1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages

 
 
 

 

Matukio ya Kisiasa | 21.11.2008

Obama sasa anaelekea kumteua Hillary Clinton kuwa waziri wa mambo ya nchi za Nje wa Marekani

Kamati kuu inayoisuka serikali ya Rais Mteule Barrak Obama nchini Marekani, inasema kuwa rais huyo mteule , sasa inaelekea kumteua Hillary Rodham Clinton, mke wa Rais wa zamani Bill Clinton.


Kamati kuu inayohusika na kuisuka serikali ya Rais Mteule Barrak Obama nchini Marekani, inasema kuwa rais huyo mteule , sasa inaelekea kumteua Hillary Rodham Clinton, mke wa aliyekuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinto katika wadhifa wa waziri wa  mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo.

 

Wasaidizi wa karibu kwenye kundi hilo linaloisuka serikali ya Barrak Obama, itakayoapishwa Januari 20 mwakani, wanasema kuwa mipango  ya kumteua Hillary Clinton imepiga hatua  kubwa baada  ya kupigwa jeki na rais wa zamani  Bill Clintonâ—„


 Baada ya kukutana  wiki iliyopita na kufanya mazungumzo ya muda mrefu huko Chicago, Rais huyo mteule Barrak Obama, anaonekana kumjongelea zaidi  Hillary Clinton ambaye alikuwa mpinzani wake wakati wa kampeini ya uteuzi wa mgombea urais wa chama cha Demokrati.


Punde tu baada ya mashauriano hayo, imebainika kwamba Barrak Obama anadhamiria kumteua Hillary Clinton katika wadhifa  wa warizi wa mambo ya Nje nchini Marekani kuchukua mahala mwa Condolizza Rice.


 Msimamo huo ambao imekuwa ikienezwa na vyombo vya habari kama uvumi tu, huenda ukatimia wiki ijayo, wakati  rais huyo mteule anapotarajiwa kumteua Hillary, mke  wa rais wa zamani nchini Marekani Bill Clinton baada ya  sherehe za chama cha Demokrat Novemba 27, kusherehekea ushindi wa  Barrak Obama.


 Ingawa Clinton hajatangaza hadharani iwapo atakubali uteuzi huo, ishara ziko wazi kwamba sasa Hillary Clinton anaelekea kuchukua wadhifa huo, baada ya  mumewe Bill Clinton kutangaza kwamba atachunguza upya,kuimarisha na kupanua shughuli za wakfu wake  wa Bill Clinton iwapo mkewe atateuliwa katika wadhifa huo.

 

Duru zinaasema kuwa pande hizo mbili zimekuwa zikifanya mazungumzo tangu siku ya Jumatatu wiki hii, kutafuta njia za kuimarisha ufadhili kwa wakfu huo wa Bill Clinton unaoendesha shughuli zake katika jumla ya mataifa 27.


 Wakati huo huo waziri wa ulinzi nchini Marekani Roberts Gate, amekutana na  kamati andalizi kuhusu masuala ya usalama katika serikali ijayo ya Barrak Obama, na kuongeza uvumi kwamba  huenda Robert Gates akasalia katika wadhifa huo katika serikali mpya ijayo ya Barrak Obama.


 Gate alikutana na  maafisa wakuu wa kamati hiyo ya Barrak Obama, John White na Michele Flournoy, na msemaji katika makao makuu ya  wizara ya Ulinzi Geoff Morrel.


 Huu ulikuwa mkutano wa kwanza baina ya waziri huyo wa ulinzi na kamati hiyo andalizi ya rais mteule Barrak Obama, ambapo kamati hiyo, pia katika hali ya kujiandaa, inatarajiwa kuchunguza maongozi, utaratibu wa utendaji kazi katika idara hiyo, kwa ushirikiano na waziri huyo wa ulinzi.


Uvumi kuhusu uteuzi wa Robert Gates katika wadhifa huo, ulianza kuenea baada ya mshauri mkuu wa Barrak Obama  kuhusu maongozi ya kigeni, Richard Danzig, kusema kuwa Robert Gates anauzoefu katika kazi hiyo na ingekuwa vyama kuhudumu katika serikali ya Barrak Obama.

 

Eric Kalume Ponda

 
Share this article

Send us an e-mailSendPrint

More on the topic



 
Picture of the Day
ImageOfTheDay

DW-TV EUROPE live

Politik direkt - Das Politikmagazin